• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Arsenal yawa kileleni mwa kundi lao michuano ya UEFA Europa League

    (GMT+08:00) 2017-09-29 08:42:47

    Jana usiku michuano ya UEFA Europa League hatua ya makundi iliendelea tena barani Ulaya, mchezo kati ya BATE Borisov dhidi ya Arsenal ni miongoni mwa michezo iliyiopigwa kwenye ligi hiyo.

    Arsenal walikuwa ugenini katika uwanja wa Borisov Arena kucheza dhidi ya wenyeji wao BATE Borisov, pamoja na Arsenal kuwa ugenini na BATE Borisove kuwazidi wapinzani wao kwa sapoti kubwa ya mashabiki wao lakini Arsenal walifanikiwa kupata ushindi wa magoli 4-2. Arsenal pia walifanikiwa kuutawala mchezo kwa asilimia 62 na BATE Borisov kuutawala mchezo kwa asilimia 38, magoli ya Arsenal yalifungwa na Theo Walcott dakika ya 9 na dakika ya 22, Robert Holding dakika ya 26 na Oliver Giroud dakika ya 49. Na yale ya BATE Borisov yalifungwa na Mirko Ivanic dakika ya 28 na Mikhail Gordeychuk dakika ya 67, ushindi huo sasa unaifanya Arsenal kufikisha jumla ya point sita na kuongoza kundi lao wakifuatiwa na Crven Zvezda wenye point nne.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako