• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Sekta ya utalii kuimarika mwishoni mwa mwaka huu

    (GMT+08:00) 2017-09-29 18:44:03

    Wadau wa sekta ya utalii nchini Kenya wamesema wana wanatarajia idadi kubwa ya wageni kutoka nje ambao watasaidia kupiga jeki sekta hiyo ambayo ilikuwa imedidimia. Taarifa hii inakuja wakati ambapo idadi ya wageni katika kipindi cha uchaguzi ilikuwa imepungua kwa asilimia 20. Hadi kufikia sasa tayari vyumba vingi vimelipiwa katika miezi ya Novemba na Disemba.Wakati huo huo baadhi ya mahoteli yamesaini mapatano na treni ya usafiri wa abiria Madaraka Express yanayolenga kupiga jeki utalii katika pwani ya Kenya.Kwa mujibu wa mapatano hayo, gharama inatarajiwa kupungua kwa asilimia 25 kati ya hoteli ya Diani Reef Beach Resort na Madaraka Express.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako