• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Dar es Salaam. Vijana wametakiwa kutopoteza muda kujadili masuala ya mikopo badala yake wajadili mawazo bora ya biashara.

    (GMT+08:00) 2017-09-29 18:44:50

    Ombi hilo limetolewa kwenye mdahalo ulioandaliwa na asasi za kiraia kwa kushirikiana na mfuko wa Maendeleo wa Aga Khan, ukilenga kuwapa vijana uelewa wa njia ya kujiimarisha katika ujasiriamali.

    Profesa Honest Ngowi, mtafiti na mshauri wa uchumi na biashara amesema vijana wengi wamekuwa wakipoteza muda kutafuta mikopo kwenye taasisi za fedha, badala ya kufikiria wazo bora la biashara ambalo watalitumia kuendeleza fedha iwapo wataipata.

    Amesema taasisi za fedha zikiwemo benki hazikopeshi vijana kutokana na kuhitaji dhamana ambazo wengi wao hawana.

    Profesa Ngowi amezitaka taasisi za fedha badala ya kusubiri mawazo ya matumizi ya fedha walizonazo kutoka kwa wakopaji, wanatakiwa kuwa na mawazo yatakayosaidia kuzizungusha fedha walizonazo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako