• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • NSSF ya Uganda yawekeza kwenye sekta ya nyumba

    (GMT+08:00) 2017-09-29 18:45:11

    Hazina ya uzeeni nchini Uganda NSSF imezindua rasmi mradi wa ujenzi wa nyumba 2740 katika eneo la Wakiso nchini Humo. Mradi huo unatarajiwa kugharimu jumla ya dola milioni 400 za kimarekani na utajengwa kwa awamu ndani ya kipindi cha miaka 10.Mkurugenzi mkuu wa NSSF Bw Richard Byarugaba amesema mradi huo unatokana na uhaba wa nyumba za kisasa kwa watu wenye maisha ya daraja la wastani na la kwanza. Byarugaba ameongeza kuwa shirika hilo limeamua kuwekeza katika sekta hiyo kwa kuwa ndiuo njia pekee ya kujizolea faida wakati kama huu.Awamu ya kwanza inatarajiwa kumalizika ndani ya kipindi cha mwaka mmoja.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako