• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mazungumzo ya kwanza kati ya China na Marekanbi kuhusu jamii na utamaduni yafanyika huko Washington

    (GMT+08:00) 2017-09-29 18:55:28

    Mazungumzo ya kwanza kati ya China na Marekani kuhusu jamii na utamaduni yamefanyika jana huko Washington, na kuendeshwa kwa pamoja na naibu waziri mkuu wa China Bi. Liu Yandong na waziri wa mambo ya nje wa Marekani Bw. Rex Tillerson.

    Bi. Liu Yandong amesema, China na Marekani zinapaswa kuheshimu njia ya kujiendeleza na utaratibu wa jamii wa upande mwingine, pia zinatakiwa kupanua ushirikiano wa ufanisi na kuwanufaisha wananchi wao.

    Kwa nyakati tofauti, Bi. Liu Yandong pia alikutana na rais Donald Trump wa Marekani. Katika mazungumzo yao, Rais Trump amesema mawasiliano ya jamii na utamaduni kati ya China na Marekani ni muhimu, na anazitaka nchi hizo mbili zipanue ushirikiano wa kirafiki kwenye sekta mbalimbali.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako