• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa China akutana na waziri wa mambo ya nje wa Marekani

    (GMT+08:00) 2017-09-30 19:21:01

    Rais Xi Jinping wa China leo hapa Beijing amekutana na waziri wa mambo ya nje wa Marekani Bw. Rex Tillerson.

    Rais Xi amesema zikiwa nchi kubwa zaidi zinazoendelea na zilizoendelea, China na Marekani ambazo zinachukua nafasi ya pili na ya kwanza duniani kwa nguvu ya uchumi, zinapaswa kuishi pamoja kwa amani, na kushirikiana na kupata mafanikio ya pamoja, ili kuwanufaisha wananchi wao, na watu wote duniani. Amesema China inatilia maanani ziara rasmi ya rais Donald Trump wa Marekani nchini China itakayofanywa mwezi Novemba.

    Bw. Tillerson ametoa salamu kwa rais Xi kwa niaba ya Rais Trump, na kusema Marekani inatilia maanani kuendeleza uhusiano kati yake na China, na kupenda kushirikiana na China, kuongeza uaminifu, mawasiliano na ushirikiano katika sekta mbalimbali, na kukabiliana na changamoto za kimataifa na kikanda kwa pamoja.

    Mjumbe wa taifa la China Bw. Yang Jiechi siku hiyo pia amekutana na Bw. Tillerson.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako