• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ligi kuu ya Uingereza – EPL: Manchester United yaua, Man City yavunja daraja la Chelsea, Arsenal yainyuka Brighton.

    (GMT+08:00) 2017-10-02 08:24:00
    Timu ya Manchester United imezidi kujiweka katika nafasi nzuri ya kutafuta ubingwa wa ligi kuu ya England baada ya kupata ushindi mnono wa jumla ya magoli 4-0 dhidi ya Crystal Palace mchezo uliopigwa kwenye dimba la Old Trafford.

    Magoli ya Man United yakifungwa na Fellaini aliyefunga mawili dakika ya 35 na 49, Juan Mata dk 3 na Lukaku 86.

    Katika uwanja wa darajani wenyeji Chelsea wamepoteza mechi yao baada ya kufungwa goli 1-0 na Manchester City. Goli la Man City limefungwa na Kevin De Bruyne kipindi cha pili kwa shuti kali na kumshinda mlinda mlango dakika ya 67 Courtois. Arsenal imeendeleza wimbi la ushindi kwa kuichapa Brighton 2-0.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako