• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uganda: Zaidi ya watu 250 wapoteza ajira baada ya kiwanda cha punda kufungwa Tororo

    (GMT+08:00) 2017-10-03 18:22:54

    Zaidi ya watu 250 nchini Uganda watapoteza ajira baada ya wizara ya kilimo nchini humo kuagiza kufungwa kwa kiwanda kipya cha nyama ya punda kilichoko wilaya ya Tororo.

    Katibu wa kudumu kwenye wizara hiyo Pius Wakabi Kasajja na maafisa kutoka kwa wilaya hili wamefunga kiwanda hicho cha Haung Cheng kwa kile walichokitaja kuwa ni kutofuatwa kwa taratibu zifaazo.

    Kiwanda hicho kilifunguliwa mwezi Aprili nyama yake na bidhaa nyinginezo zikipelekewa nchini Vietnam.

    Wakaazi pia wamekuwa wakilalamika kwamba kiwanda hicho hakijatimiza viwango vinavyotakiwa vya usafi.

    Hata hivyo kamishena wa wilaya ya Tororo Martin Orochi, amepinga hatua hiyo akisema kinahatarisha uhusiano mzuri kati ya wawekezaji na serikali.

    Alisema maafisa wa wizara husika kwanza wangeshauriana kwanza na wawekezaji kabla ya kuchukua hatua hiyo ili kutafuta suluhu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako