• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Shirika la ndege la Afrika Kusini latafuta baadhi ya safari kwenda Uganda, DRC na Angola

    (GMT+08:00) 2017-10-03 18:23:19

    Shirika la ndege la Afrika Kusini litafuta safari yake moja kwenye Uganda sasa ikisalia na safari 6 kwa wiki kuanzia Oktoba 29.

    Mkurungezi wa shirika hilo nchini Uganda Yogi Birigwa, amasema kuondolewa kwa safari hiyo moja hakutaathiri oparesheni zake kwenda Entebbe.

    Alisema soko la Uganda kwa shirika hilo linasalia kuwa muhimu na hivyo safari sita hizo zitakuwa Jumatatu, Jumanne, Jumatano, Ijumaa, Jumamosi na Jumapili.

    Shirka hilo lina madeni ya rand bilioni 7 na lilitakiwa na mahakama kulipa Citibank rand bilioni 1.9 ifikapo mwishoni mwa Septemba miezi miwili tu baada ya kupokea msaada wa rand bilioni 2 kiutoka kwa serikali.

    Aidha safari za shirika hilo kwenda Luanda zitapunguzwa kutoka 7 hadi 4 kwa wiki na zile za kwenda Kinshasa kupunguzwa kutoka 6 hadi 5.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako