• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Zimbabwe yatarajia watalii kutoka China

  (GMT+08:00) 2017-10-03 18:35:09

  Maonesho ya kimataifa ya utalii ya Sanganai, ambayo ni maonesho makubwa zaidi ya utalii nchini Zimbabwe, yamefanyika kuanzia tarehe 27 Septemba hadi tarehe mosi Oktoba mjini Lavayo, Zimbabwe. Akihojiwa na mwandishi wetu, Waziri wa utalii wa nchi hiyo Bw. Walter Mzemb amesema, Zimbabwe yenye vivutio vingi vizuri vikiwemo maporomoko ya maji ya Victoria, na mabaki ya kale ya Zimbabwe, inawakaribisha watalii kutoka China.

  Utalii ni moja ya nguzo nne za uchumi wa Zimbabwe, na kuchangia asilimia 10 ya thamani ya uzalishaji mali nchini humo. Wageni wanaotalii nchini Zimbabwe wengi wao wanatoka nchi za magharibi na nchi jirani barani Afrika, wachina bado ni wachache. Bw. Mzemb amesema anatarajia watalii wengi zaidi kutoka China watatembelea Zimbabwe. Kwani nchi hiyo ina vivutio vingi vya utalii, aidha ina amani, utulivu wa kudumu na watu wakarimu. Anasema,

  "Takwimu zilizotolewa na China zinaonesha kuwa kati ya mwaka 2015 na 2016, idadi ya wachina waliotalii katika nchi za nje ilikuwa zaidi ya milioni 128, kati yao milioni 1.5 walikuja Afrika, ambapo wale waliokuja Zimbabwe walikuwa kati ya elfu 15 na 30 tu. Hatuwezi kuridhika na idadi hiyo ndogo. Tunatumai kuwa hadi kufikia mwaka 2020, idadi ya wachina wanaotalii nchini kwetu itafikia laki tano kwa mwaka."

  Ili kutimiza lengo hili, Zimbabwe imechukua hatua mbalimbali. Bw. Mzemb ameeleza kuwa raia wa China wanaruhusiwa kuomba viza baada ya kufika kwenye ardhi ya Zimbabwe, pia Shirika la Ndege la Zimbabwe linashughulikia kurejesha tena safari za ndege za moja kwa moja kati ya Harare na Beijing.

  Shirika la Ndege la Zimbabwe lilianzisha safari za ndege ya moja kwa moja kati ya Harare na Beijing mwaka 2004 na kati ya Harare na Guangzhou mwaka 2007, lakini kutokana na ukosefu wa uendeshaji bora, zilisimamishwa baadaye. Bw. Mzemb amesema, safari za ndege za moja kwa moja kati ya Zimbabwe na China zinatarajiwa kurejeshwa ndani ya miezi sita. Anasema,

  "Tunawasiliana na mashirika mapya yanayotarajiwa kushirikiana nasi. Naamini safari za ndege za moja kwa moja kati ya nchi zetu zitarejeshwa ndani ya miezi sita."

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako