• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uganda kuuzia umeme Sudan kusini,DR Congo

    (GMT+08:00) 2017-10-04 19:38:41

    Serikali za Uganda na Sudan kusini zimetia saini makubaliaono ya kuvuka mipaka yatakayoruhusu Uganda kuongeza umeme ndani ya miji ya mipakani ya Sudan Kusini ya Kaya na Nimule.

    Akizungumza wakati wa utiaji saini jana jijini Kampala,Waziri wa Nishati Simon D'Ujanga alisema nchi hizo mbili zinatekeleza mkataba wa uchangiaji wa umeme wa Afrika Mashariki ambao unashinikiza nchi wanachama kuunganisha umeme baina yao kulingana na ukaribu.

    Aliongeza kuwa Uganda tayari inatekeleza uunganishaji umeme katika mipaka huku Rwanda na Tanzania zikitoa huduma za umeme kwa mji wa Rakai na Uganda itaunganisha umeme mashariki mwa DR Congo.

    D'Ujanga aliongeza kuwa baada ya kutia saini mkataba wa makubaliano na Suda kusini,nchi zote mbili zinaounda kamati ya kiufundi ili kutathmini ukubwa wa kazi,kwa sababu Uganda tayari ishaunganisha umeme katika miji ya Nimule na Kaya lakini upande wa Uganda.

    Waziri wa Umeme na Mabwawa wa Sudan kusini,Dkt Dhiev Mathok Diing Wol, ambaye alitia saini kwa niaba ya serikali yake alisema mkataba huo unatimiza makubaliano ya viongozi wa kikanda wa kuunganisha umeme katika miji ya mipakani ili kukuza shughuli za kibiashara katika miji ya mipakani,na kupunguza uhamiaji wa wakimbizi nchini Uganda.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako