• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya-KEPSA yaonya uchumi kudorora kufuatia joto la kisiasa Kenya

    (GMT+08:00) 2017-10-04 19:39:20

    Jamii ya wafanyabiashara nchini Kenya imesema kuwa joto la kisiasa nchini humo linaathiri uchumi.

    Chini ya mwavuli wa Umoja wa Wafanyabiashara Binafsi nchini Kenya (Kepsa) kundi hilo linadai kuwa hali ya atiati ya kisiasa sasa ni tishio kwa uchumi na maendeleo ya nchi.

    Kepsa inasema huenda kukashuhudiwa viwanda vingi kufungwa nchini Kenya,makongamano ya kimataifa yakafutwa,na kuathiri moja kwa moja utalii na kuongeza ukosefu wa ajira.

    Kepsa inasema kuwa pato la taifa la Kenya katika kipindi cha miezi sita iliyopita limeshuka hadi asilimia 5 katika kipindi cha uchaguzi,jambo ambalo linatarajiwa kuathirikia zaidi wakati wa uchaguzi mpya tarehe 26 mwezi huu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako