• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania:Magufuli anunua ndege 6

    (GMT+08:00) 2017-10-04 19:39:42

    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe Dkt. John Pombe Magufuli amesema serikali ya Tanzania imenunua ndege sita ikiwepo ndege moja yenye uwezo wa kutoka Dar es salaam hadi Marekani moja kwa moja na ndege hizo zitakuja mwakani 2018, huku akiwataka watanzania kuunga mkono juhudi zake kwani anafanya hivyo kwa ajili ya kutengeneza Tanzania mpya.

    Rais Magufuli amesema hayo kwenye Mkutano wa 33 wa Jumuiya Ya Tawala za Mitaa (ALAT) ambao umefanyika leo katika Ukumbi wa Mikutano wa Mwalimu Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam.

    Amesema ndege mbili zimeshawasili Tanzania, huku nyingine nyngine ikiwepo Bombardier zitawasili mwakani 2018 mwanzoni.

    Tanzania inalenga kuboresha uchumi wa nchi hiyo.

    Hatua hii inalenga aidha kuongeza idadi ya watalii wanaoingia kwenye nchi hiyo iliyo ya pili kwa kuwa na vivutio vingi duniani lakini idadi ya watalii wanaoingia ni ndogo.

    Kwa upande mwingine Rais Magufuli amewaonya watumishi wa umma wakiwemo wakurugenzi wenye tabia za ulevi na kuwambia waache tabia hiyo mara moja kabla ya kuwatumbua.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako