• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wizara ya Kilimo Rwanda yazindua mradi wa kutathmini athari za uwekezaji katika sekta ya kilimo

    (GMT+08:00) 2017-10-04 19:40:03

    Wizara ya Kilimo nchini Rwanda imezindua mradi wa miaka mitatu ambao unalenga kutathmini athari za uwekezaji katika sekta ya kilimo,hasa kwa maisha ya wakulima na maendeleo ya kijamii na kiuchumi.

    Katibu Mkuu katika Wizara ya Kilimo Rwanda Jean Claude kayisinga amesema "mradi wa kuongeza ushahidi katika utungaji sera za kilimo "utafanywa chini ya ushirikiano wa wizara ya kilimo,benki ya dunia,na umoja wa ulaya.

    Alisema mradi huo utalenga kuhusu athari za miradi kama vile umwagiliaji,barabara za vijijini,uhifadhiu maji,ufadhili wa vijijini,miongoni mwa manmbo mengine.

    Aliongeza kuwa mradi huo utahusisha uundaji wa sera pamoja na kuboresha programu za sekta ya kilimo ambazo zinalenga kuimarisha uzalishaji na kuboresha hali za wakulima.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako