Wanariadha wawili raia wa Kenya wametajwa kuwania tuzo za dunia kwa mwaka 2017 hivyo kuifanya nchi hiyo kuwa taifa pekee kutoka Afrika Mashariki kuingiza wanariadha katika tuzo hizo. Elijah Manangoi ni mwanariadha pekee kutoka Kenya ambaye ametajwa kwenye orodha ya wanariadha 10 wa kiume na Hellen Obiri ambaye yumo katika orodha ya wanariadha kumi wa kike wanaowania tuzo hiyo.
Mbali na wakenya hao, pia yumo Muethiopia mmoja ambaye ni Almaz Ayana pamoja na wanariadha watatu kutoka Afrika Kusini akiwemo Caster Semenya.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |