• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya:Serikali kutumia sh bilioni 6 kama ruzuku ya mahindi

    (GMT+08:00) 2017-10-05 18:37:59

    Serikali ya Kenya itatumia shilingi bilioni 6 kama ruzuku ya mahindi ili kuendeleza biashara ya mahindi ya bei rahisi.

    Rais Uhuru Kenyata amesema pesa hizo zitatumika kununua mahindi yote ya wakulima katikia msimu huu wa mavuno chini ya mpango wa serikali wa kuhifadhi chakula ili kuhakikisha kuna usalama wa chakula.

    Uhuru amewahakikishia wakenya kwamba bei ya mahindi ya kilo 2 itasalia shilingi 90 na kuwataka kuondoa hofu ya uwezekano wa kupanda maradufu kwa bei ya unga.

    Wizara ya kilimo aidha imeahidi wakulima kupata mbolea ya bei nafuu ya shilingi 1200 kutoka 1800 kwa kilo 50 ya gunia la mahindi.

    Katika harakati ya kukabiliana na baa la nchini Kenya ,serikali imetenga bajeti ya shilingi bilioni 30 kwa wizara ya kilimo ili kutekeleza miradi ya maendeleo na ukuzaji wa kilimo cha biashara kwa wakenya.

    Kilimo nchini Kenya sasa kinatumiwa kama kitega uchumi muhimu kwa vijana na kina mama.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako