• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania:Serikali yahimizwa kuongeza mishahara ya wafanyikazi

    (GMT+08:00) 2017-10-05 18:41:43

    Chama cha ACT-Wazalendo kimelitaka Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi(Tucta)kupinga hatua ya serikali kuzuia nyongeza ya mishahara kama ilivyokuwa inafanya huko zamani.

    Hii ni baada ya kupita siku moja tangu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Pombe John Magufuli kusema hataongeza mishahara kwa wafanyakazi.

    Katibu wa Itikadi, Mawasiliano na Uenezi wa ACT, Ado Shaibu amesema Chama cha ACT Wazalendo kimesikitishwa na baadhi ya kauli zisizo za kiuongozi zilizotolewa, Oktoba 3, 2017 na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

    ACT Wazalendo tunao wajibu wa kuwakumbusha watu hao juu ya kufuata Katiba ya nchi, kuacha kauli zisizo za kiuongozi, pamoja na kutokujiona ni wafalme wanaoweza kufanya chochote watakacho.

    Maelezo yao yamejikita kwenye masuala Kupandisha Mishahara ya Wafanyakazi wa sekta ya Utumishi wa wakielezea kwamba wanastahili nyongeza kutokana na mchango wao madhubuti katika ujenzi wa Taifa kwenye sekta mbalimbali, kwa utumishi wao wa kutukukakwani wafanyakazi ndio wanaochangia zaidi mapato ya serikali kuliko waajiri wao.

    Kitabu cha Mapato ya Serikali Kuu cha mwaka 2016/17 kinaonyesha kuwa Wafanyakazi wote wa sekta ya Umma na Sekta Binafsi watachangia jumla ya shilingi trilioni 3 kwenye mapato yote ya Serikali kulinganisha na wenye mitaji (waajiri) ambao watachangia jumla ya shilingi bilioni 900 tu kutoka kwenye kodi za faida/gawio, ongezeko la mitaji na riba (taxes on income/interests, profits and capital gains).

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako