• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rwanda:Rwanda yatangaza vita vikali dhidi ya biashara ya binadamu

    (GMT+08:00) 2017-10-05 18:42:03

    Shirika la kukabiliana na uhalifu wa kimataifa la Interpol limetoa onyo kali dhidi ya walanguzi wa binadamu nchini Rwanda.

    Hatua hii inajiri kufuatia kukithiri kwa biashara ya uuzaji wa binadamu kutoka Rwanda hadi nchi za nje.

    Shirika la Umoja wa Mataifa la United Nations Office and Crime limetahadhirisha nchi za eneo la jangwa la Sahara kuhusiana na ongezeko la biashara hiyo.

    Biashara hii imethibitishwa kufanyika kupitia kwa kusajiliwa watu kwa udanganyifu,kusafirishwa ,kuibwa na kutishwa maisha kabla ya kuzwa kwa watu binafsi ,kulazimishwa kufanya biashara za ukahaba na hata kuuwawa kwa ajili ya viungo vya miili.

    Takwimu zinaonyesha kwamba watu zaidi 2580 waliohusika kwenye biashara hiyo mwaka 2016 ni raia wa sub sahara.

    Kamishena mkuu wa Interpol Rwanda Peter Karake ametishia kuchukua hatua kali ikiwemo sheria mpya za kuwakamata wafanyibiashara hao wa ulanguzi wa binadamu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako