• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mwanasoka Kolo Toure awa kocha msaidizi wa Ivory Coast

    (GMT+08:00) 2017-10-06 09:01:50

    Mwanasoka wa zamani wa kimataifa wa klabu ya Arsenal ya Uingereza Kolo Toure, amepewa shavu na taifa lake la Ivory Coast baada ya jana kumtangaza kuwa kocha msaidizi wa timu ya taifa ya Ivory Coast. Katika mechi ya leo kati ya Ivory Coast na Mali ya kuwania kufuzu kucheza michuano ya Kombe la Dunia, Kolo Toure atakuwa katika benchi kama kocha msaidizi akimsaidia kocha Wilmots. Toure ambaye katikati ya mwezi September kocha wake wa Celtic Brendan Rodgers alimchagua kuwa msaidizi wake, ameendelea kuaminika na kupata nafasi kubwa katika nchi yake.

    Kolo Toure mwenye umri wa miaka 36 alianza soka katika klabu ya Asec-Mimosas ya kwao Ivory Coast na baadae akacheza vilabu vya Ulaya kama Arsenal, Man City na Liverpool.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako