• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Bayern Munich kumrejesha kocha wake wa zamani Jupp Heynckes

    (GMT+08:00) 2017-10-06 09:03:08

    Bayern Munich imeripotiwa kujipanga kumrejesha kocha wake wa zamani Jupp Heynckes ili kuchukua nafasi ya Carlo Ancelotti ambaye ametimuliwa mwezi uliopita. Jupp Heynckes aliiongoza Bayern kutwaa mataji matatu yani Trebble msimu wa 2012/13 na baada ya hapo aliachia ngazi na kuchukua mapumziko. Bayern imejipanga kumpa mkataba wa muda mfupi kocha huyo ili akiongoze kikosi hicho hadi mwisho wa msimu huu. Endapo Heynckes atarudi Bayern, itakuwa ni mara yake ya nne kuifundsha timu hiyo ambapo mara ya kwanza ilikuwa ni 1987-1991 kisha 2009 na 2011-2013. Hivi sasa Bayern ambayo ina alama 14 baada ya mechi 7 nyuma ya Borrusia Dortmund yenye alama 19 ipo chini ya kocha Willy Sagnol ambaye alikuwa msaidizi wa Ancelotti.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako