• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kombe la dunia mwaka 2030 nchi kadhaa zaanza kupigana vikumbo

    (GMT+08:00) 2017-10-06 09:05:46
    Mataifa matatu kutoka America Kusini ya Argentina, Uruguay na Paraguay yamejiandaa kuungana na kuwa kitu kimoja kwa ajili ya kuwa mwenyeji wa michuano ya kombe la dunia mwaka 2030.

    Marais wa nchi hizo tatu waliweka kikao kwa pamoja kujadili mambo mbali mbali ya mataifa hayo na ndipo wakaja na hoja moja ya kuungana. Wakati nchi hizo zikijipanga, hapa barani Asia, China nayo imeonesha nia ya kuandaa michuano hiyo mikubwa duniani. Mbali na China, UEFA nayo mwezi July mwaka huu walisema michuano ya mwaka 2030 itakuwa jambo kubwa sana kwao na kwamba wao kama Ulaya watawapa ushirikiano mkubwa Uingereza.

    Michuano ijayo ya kombe la dunia itapigwa nchini Urusi mwakani huku baada ya hapo taifa la Qatar litaandaa michuano ya kombe la dunia mwaka 2022 na kisha Mexico – USA na Canada wakijipanga kwa 2026 ambapo Morocco nao wanaitaka.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako