• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Hatima ya EAC kusaini mkataba wa ushirikiano wa kibiashara kujulikana mwezi ujao

    (GMT+08:00) 2017-10-06 18:24:01

    Hatima ya nchi za Jumuiya ya Afrika mashariki (EAC) kusaini mkataba wa ushirikiano wa kibiashara (EPA) kati ya nchi hizo na nchi za umoja wa ulaya (EU), sasa inatarajiwa kujulikana mwezi ujao wakati wa kikao cha wakuu wa nchi za EAC.

    Mwenyekiti wa EAC ambaye pia ni rais wa Uganda, Yoweri Museveni alinukuliwa akisema hayo kwenye mkutano na rais wa Tume ya Ulaya, Jean-Claude Juncker. Museveni aliwasilisha mawazo ya nchi wanachama ikiwemo Tanzania ambayo ilionesha kutokuwa tayari kusaini mkataba huo ikisema haujali maslahi ya nchi za EAC. Mkutano huo ulilenga kujadili nafasi ya kiuchumi ya EAC na pia kutoiadhibu Kenya kutokana na nchi wanachama kutosaini mkataba huo.

    Kwenye mkutano huo, Museveni aliandama na katibu mkuu wa EAC Liberat Mfumukeko, mawaziri wa biashara kutoka nchi wanachama. Kwa upande wake, katibu mkuu wa wizara ya ushirikiano wa Afrika Mashariki ya Kenya Betty Maina amemshukuru Museveni kwa kuitetea Kenya kwa Umoja wa Ulaya kutoiadhibu Kenya.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako