• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Benki ya Dunia kufadhili masomo ya Sekondari Kenya

    (GMT+08:00) 2017-10-06 18:24:17

    Benki ya dunia inatarajiwa kutoa jumla ya shilingi bilioni 20 kufadhili masomo ya sekondari nchini Kenya kuanzia mwaka ujao.Makubaliano hayo yalitsainiwa na benki hiyo pamoja na maofisa wa wizara ya fedha ya Kenya.Mkurugenzi mkuu wa Taasisi ya mtaala wa elimu Bw Julius Jwan amesema fedha hizo zitaelekezwa kwenye ufadhili wa mafunzo ya masomo ya sayansi na lugha hasa katika maeneo yaliyotengwa.Akizungumza mjini Nairobi,Bw Jwan amesema mtaala mpya wa masomo unatarajiwa kutolewa hivi karibuni lakini akasisitiza kuwa wadau wameona hakuna haja ya kuutupilia mbali mfumo wote wa elimu ya 8.4.4. Benki kuu imesema lengo la hatua hiyo ni kuhakikisha Kenya inafikia lengo lake kufikia ruwaza ya mwaka wa 2030.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako