• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Serikali yawataka wakazi wa Shinyanga kujiandaa kupokea fursa zinazojitokeza

    (GMT+08:00) 2017-10-06 18:26:26

    Waziri wa habari, utamaduni, sanaa na michezo Bw. Harrison Mwakyembe amewataka wananchi wa Shinyanga kujiandaa kupokea fursa mpya zinazojitokeza ikiwemo ujenzi wa bomba la mafuta litakalopita Shinyanga kutoka Uganda hadi Tanga.

    Mwakyembe aliyasema hayo alipokuwa akifungua rasmi jukwaa la biashara mkoani Shinyanga lililoandaliwa na Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN) kwa kushirikiana na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga.

    Mwakyembe amesema kwa kuzingatia hali ilivyo mkoani humo, wakaaji wa Shinyanga wamekuwa wakipitwa na na fursa zinazotokea katika eneo hilo na badala yake zinachukuliwa na wageni. Mwakyembe ameongeza kuwa wakazi wa Shinyanga wasipojiandaa, watajikuta fursa nyingi zinazotangazwa na kuibuliwa zikichukuliwa na wageni wakiwemo hata kutoka nje ya nchi.

    Shinyanga inapakana na nchi jirani zikiwemo Rwanda, Burundi, Uganda na Kenya.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako