• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • EACC kuanza kutekeleza sheria ya kumaliza Rushwa ifikapo mwaka ujao

    (GMT+08:00) 2017-10-06 18:36:51

    Tume ya kupambana na ufisadi nchini Kenya imeanza kutekeleza sheria mpya ya kupambana na rushwa ili kufanikisha juhudi za kupambana na ufisadi. Sheria hiyo ya mwaka wa 2016 ambayo ilisainiwa na rais Uhuru Kenyatta Disemba mwaka wa 2016 inawalenga wahalifu wanaotoa au kupokea rushwa katika sekta ya kibinafsi.Mkurugenzi wa shirika hilo Vincent Okong'o amesema ufisadi umeota mizizi nchini Kenya lakini watahakikisha tabia hiyo inatokomea nchini Kenya.Okong'o alikuwa akisema hayo baada ya kufanya mkutano na wadau wa sekta ya usafiri kutoka maeneo ya mgharibi katika hoteli ya Kisumu hiyo jana.Amesema ufisadi pia umeota mizizi katika sekta ya usafiri ambapo jumla ya shilingi bilioni 3 hutolewa kila mwaka kama rushwa .Hadi kufikia sasa tume ya kupambana na ufisadi imeshughulikia jumla ya kesi 316 katika sekta hiyo na tayari maofisa wa polisi 145 wameshtakiwa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako