• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China imejenga vyuo 516 vya Confucius katika nchi 142 duniani

    (GMT+08:00) 2017-10-06 18:37:43

    China imejenga vyuo 516 na madarasa zaidi ya 1,000 ya Confucius vinavyolenga kufanya mawasiliano na utamaduni katika nchi 142 duniani, ambapo hadi sasa vimefundisha wanafunzi zaidi ya milioni 7.

    Ili kueneza lugha ya Kichina na kuinua ushawishi wa utamaduni wake duniani, mwaka 2004 China ilianza kujenga chuo cha Confucius katika nchi za nje kwa madhumuni ya kufundisha lugha ya Kichina na kueneza utamaduni wa China. Naibu mkuu wa makao makuu ya vyuo vya Confucius Bw. Ma Jianfei amesema vyuo vya Confucius vimepiga hatua kubwa katika miaka 13 iliyopita, na hadi sasa vimefundisha wanafunzi zaidi ya milioni 7.

    "Hadi sasa tumejenga vyuo 516 na madarasa 1,076 ya Confucius katika nchi 142 duniani, ambavyo vimefundisha wanafunzi zaidi ya milioni 7, huku shughuli tulizoandaa za kueneza utamaduni wa China zikiwashirikisha watu karibu milioni 100. Vyuo vya Confucius vimewafurahisha watu wa nchi mbalimbali duniani."

    Etel Vinicius ni mwanafunzi wa chuo cha Confucius cha Chuo Kikuu cha Minas Gerais cha Brazil, jina lake la Kichina ni Zhang Sizhe. Amepata tuzo ya kusomea China kwa mwaka mmoja. Anasema,

    "Nilianza kujifunza lugha ya Kichina mwezi Machi mwaka jana. Walimu wetu kutoka China wote ni vijana, na kwa kawaida muhula wao ni mwaka mmoja tu. Mbali na lugha, pia wanatufundisha mambo mengine kuhusu China, kama vile vyakula, mila na desturi. Kila chuo cha Confucius kinaandaa shughuli za utamaduni, zikiwemo kaligrafia na Kongfu. Siku moja tulishiriki shughuli ya kutengeneza vyakula vya China, na nilitengeneza Baozi, hii ni mara yangu ya kwanza kuonja Baozi."

    Kutokana na maendeleo ya uchumi wa China na mahitaji ya kuwasiliana na China, nchi mbalimbali duniani zinazingatia umuhimu wa lugha ya Kichina. Hadi sasa nchi 67 zimeweka mafunzo ya lugha ya Kichina kwenye mfumo wao wa elimu, na nchi zaidi ya 170 zimeanzisha kozi au madarasa ya lugha hiyo.

    Bw. Paul Burton Bell ni mkurugenzi mtendaji wa chuo cha Confucius cha Chuo Kikuu cha Oklahoma cha Marekani. Amesema chuo hicho cha Confucius kilianzishwa miaka 11 iliyopita, na kuleta fursa nzuri kwa watu kuelewa zaidi mambo ya China.

    "Tunaweza kufundisha lugha ya Kichina bila ya chuo cha Confucius, lakini tukikosa chuo hicho, wanafunzi wetu 76 hawatapata tuzo ya kusoma katika vyuo vikuu nchini China, walimu wetu 50 watakosa fursa ya kwenda China kuelewa mfumo wao wa elimu, tutashindwa kuwapata walimu na wanafunzi 130 kutoka China kutufundisha utamaduni na lugha ya China, wanafunzi zaidi ya 150 wa shule ya sekondari ya Oklahoma hawatapata nafasi ya kushiriki shughuli ya daraja la lugha ya Kichina linalofanyika nchini China, na sisi pia hatutaweza kutafsiri vitabu 9 vya China, ili kujulisha waandishi hodari wa China akiwemo Mo Yan aliyepata tuzo ya Nobel."

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako