Siku ya Ijumaa, Benki Kuu ya Kenya ilibainisha kwamba SBM itachukua zaidi ya asilimia 75 ya Sh bilioni 76 iliyoshikiliwa katika akaunti zilizozuiwa ndani ya Benki ya Chase.
Kulingana na Gavana wa, Benki Kuu ya Kenya (CBK) Patrick Njoroge, wateja walikuwa wameweka fedha na benki hiyo watapata sh bilioni 57 kuanzia Januari 1, 2018, lakini katika awamu tatu ambazo zitaenda hadi 2021.
Njoroge hakutoa mwelekeo wowote kwa Sh bilioni 19 iliyobaki katika Benki ya Chase Bank , jambo ambalo limewaacha wateja wa Benki hiyo na hofu ya watapoteza akiba zao.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |