• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kuelekea kombe la dunia 2018 bara la Afrika: Misri imekuwa timu ya pili kufuzu

    (GMT+08:00) 2017-10-10 08:57:44

    Timu ya taifa ya Misri usiku wa October 8 mwaka huu imeingia katika historia nyingine kwa kuwa timu ya pili kutokea Afrika kufuzu kucheza Kombe la dunia 2018 nchini Urusi kwa kuifunga timu ya taifa ya Congo Brazzaville kwa magoli 2-1.

    Magoli ya timu ya taifa ya Misri yamefungwa na Mohamed Salah aliyefunga magoli mawili dakika 64 na dakika za nyongeza kwa mkwaju wa penati, hiyo ni baada ya dakika ya 87 Congo kusawazisha goli la kwanza kupitia kwa Arnold Bouka Mouttou, hivyo Misri walilazimika kusubiri hadi dakika za nyongeza kukata tiketi.

    Hadi sasa timu zilizofanikiwa kufuzu kushiriki michuano ya Kombe la dunia 2018 itakayochezwa nchini Urusi ni pamoja na Urusi ambaye ni mwenyeji, Brazil, England, Iran, Nigeria, Japan, Mexico, Costa Rica, South Korea, Saudi Arabia, Ujerumani, Hispania na Poland.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako