• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Kikapu: Kings yatwaa ubingwa wa kikapu wa B'Ball kitaa

  (GMT+08:00) 2017-10-10 09:00:37

  Timu ya kikapu ya Kings imetwaa ubingwa wa mashindano ya kikapu ya B'Ball Kitaa kwa kuifunga Scorpion kwa pointi 70 kwa 60 kwenye mchezo wa fainali uliofanyika kwenye viwanja vya Soweto, Arusha.

  Kwa ushindi huo timu ya Kings licha ya kuzawadiwa Kombe, pia itaghalamiwa safari ya kuelekea Jijini Dar es Salaam kwenye michuano ya B'Ball Kitaa ya kitaifa itakayofanyika hapo badaaye mwaka huu.

  Kings iliingia katika hatua hiyo baada ya kuilaza Hooperz katika mchezo wa nusu fainali kwa vikapu 58 kwa 42, huku timu ya Scorpion ikiilaza Palllot kwa vikapu 66 kwa 47.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako