• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Uzoefu wa China kwenye kupunguza umaskini waigwa na dunia

  (GMT+08:00) 2017-10-10 16:38:49

  Mkutano wa ngazi ya juu wa kupunguza umaskini na kupata maendeleo umefanyika jana hapa Beijing. Ikiwa nchi iliyotoa mwito wa kupunguza umaskini na nguvu kubwa ya kuhimiza shughuli za kupunguza umaskini duniani, China imepata mafanikio makubwa, na uzoefu wa China kwenye kupunguza umaskini unaigwa na nchi nyingine duniani.

  Naibu waziri mkuu wa China Bw. Wang Yang jana ameshiriki kwenye ufunguzi wa mkutano huo. Amesema kuondokana na umaskini ni matumaini ya pamoja ya binadamu wote, pia ni mada muhimu ya dunia ya hivi sasa. Anasema,

  "China inapenda kushirikiana na nchi mbalimbali kufanya mawasiliano kuhusu uzoefu wa kupunguza umaskini, kuhimiza ushirikiano wa kimataifa kwenye kupunguza umaskini na kupata maendeleo, na kutilia nguvu kubwa ili kutimiza lengo la ajenda za maendeleo endelevu za mwaka 2030."

  Mafanikio iliyopata China yamesifiwa na pande mbalimbali. Mkurugenzi mkuu wa shirika la chakula na kilimo la Umoja wa Mataifa Bw. Jose Graziano da Silca ameona kuwa, asilimia ya 80 ya watu maskini duniani wako vijijini, ambao ni lengo kuu la shughuli za kupunguza umaskini, na uzoefu wa China kwenye kupunguza umaskini vijijini ni mfano mzuri. Anasema,

  "China inahimiza maendeleo ya kilimo bila kusita, na kuinua kiwango cha maisha ya watu maskini kwa kiasi kikubwa. Katika miaka 30 iliyopita, China imewasaidia watu milioni 700 kuondokana na umaskini. Sisi tunaisifu China kwa kuweka lengo lake la kupunguza umaskini, ambalo limewekwa kabla ya miaka 10 kuliko lengo la ajenda za maendeleo la mwaka 2030 la Umoja wa Mataifa. Na uzoefu wa China unatakiwa kuigwa na nchi nyingine kwa kupitia mfumo wa ushirikiano kati ya kusini na kusini. "

  Naibu katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa ambaye ni naibu mkurugenzi wa shirika la mpango wa maendeleo la umoja huo Bw. Tegegnework Gettu kwenye ufunguzi wa mkutano huo amesoma barua ya katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Antonio Guterres. Kwenye barua yake Bw. Guterres amesema, kupunguza umaskini kwa malengo madhubuti ni njia ya pekee ya kutimiza lengo la ajenda za maendeleo endelevu la mwaka 2030. Amesema siku zote China inafanya juhudi kukabiliana na changamoto, na kutekeleza mfumo wa kujiendeleza kwa pande zote. Ameeleza imani yake kuwa China itaendelea kupunguza idadi ya watu maskini, kupunguza pengo kati ya matajiri na maskini, kati ya miji na vijiji, kati ya sehemu za mashariki za pwani na sehemu za ndani za nchi kavu. Amesema uzoefu wa China unaweza kuigwa na nchi nyingine zinazoendelea.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako