• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Uganda: Bei ya umeme yapungua Uganda

  (GMT+08:00) 2017-10-10 19:01:04

  Mamlaka ya Udhibiti wa Umeme nchini Uganda (ERA) imepunguza gharama ya huduma hiyo kwa wenye biashara za ususi, maduka na vibanda kutoka Shilingi 686 hadi 685 kwa kila kizio (yaani Unit) ikiwa ni punguzo la shilingi moja.

  Hili ni punguz0 la pili kwa miezi minne.

  ERA pia imepunguzia ushuru maduka makubwa, migahawa na kliniki kutoka Shs 619.9 hadi 619.1.

  Zaidi ya hayo, ilipunguza ushuru kwa watumiaji wa viwanda vikubwa kwa Shs368.1 kutoka Shs369 na ya watumiaji wa viwanda vya ziada hadi Shs364.6 kutoka Shs365.8.

  Manispaa na mamlaka ya jiji watalipa Shs0.5 chini kwa kila kitengo kilichotumiwa kwa taa za barabara.

  Katika taarifa ya vyombo vya habari Oktoba 7, afisa mkuu wa ERA, Ziria Tibalwa Waako, alisema kuwa bei za rejareja zilingatia mfumuko wa bei, kiwango cha ubadilishaji na bei ya mafuta.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako