• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Kenya: Matumizi ya dizeli Kenya yashuka kwa mara ya kwanza katika miaka saba

  (GMT+08:00) 2017-10-10 19:04:15

  Matumizi ya dizeli nchini Kenya yameshuka kwa mara ya kwanza katika miaka saba, ikiwa ni ishara ya kushuka kwa kwa uzalishaji kwa viwanda vinavyotumia kawi ya dizeli kama vile mashine za kilimo na magari ya kibiashara.

  Takwimu za sekta hiyo zinaonyesha kuwa matumizi ya dizeli yalipungua hadi lita bilioni 1.24 katika miezi sita ya kwanza ya mwaka huu ikilinganishwa na lita bilioni 1.25 kipindi sawa na hicho mwaka jana.

  Matumizi ya dizeli ya Kenya yamekuwa yakiongezeka tangu mwaka 2011, kutokana na kuongezeka kwa mahitaji kutoka sekta muhimu za uchumi.

  Kushuka kwa matumizi kumechangiwa na ukame wa muda mrefu, na kuondolewa kwa malori kutoka barabara za Kenya na wafanyabiashara kutoka Uganda na Rwanda na badala ytake kutumia Tanzania kutokana na uchaguzi na kipidi cha siasa nchini Kenya.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako