• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Kenya: Bei ya chakula cha Mifugo Kenya kupanda

  (GMT+08:00) 2017-10-10 19:04:42

  Bei ya chakula cha Mifugo nchini Kenya inatarajiwa kupanda zaidi katika miezi ijayo,kutoka na kupanda kwa bei za malighafi muhimu kama ngano na keki ya alizeti.

  Bei ya kilo ya wishwa wa ngano imeongezeka hadi Sh19 kutoka Sh15 mwezi mmoja uliopita huku nayo kilo moja ya keki ya alizeti ikipanda kutoa shilingi 20 hadi 23.

  Kuongezeka kwa bei ya keki ya alizeti kunahusishwa na mavuno machache nchini Tanzania, ambayo ni soko la msingi la Kenya kwa ajili ya malighafi.

  Utafiti wa shirika la Kenya Market Trust wiki iliyopita ulionyesha kuwa asilimia 90 ya chakula cha mifugo kwenye soko ni bandia kwani baadhi ya wasindikaji wanaepuka kupeleka bidhaa zao kwa mamlaka ya Viwango ya Kenya.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako