• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Tanzania yakabiliwa na uhaba mkubwa wa magunia

  (GMT+08:00) 2017-10-10 19:05:07

  Tanzania inakabiliwa na uhaba mkubwa wa magunia ya katani yanayotumika kusafirishia kahawa iliyokobolewa nje ya nchi.

  Uhaba huo unaelezwa kutokana na kusimamishwa ghafla kwa uzalishaji msimu wa 2017/18 na Kampuni ya Mohammed Enterprises (MeTL), ambayo ni mzalishaji pekee.

  Ofisa Mwandamizi wa MeTL anayeshughulikia uzalishaji wa magunia, Ndekirwa Nyari alikiri kuwapo upungufu huo lakini akabainisha kuwa uzalishaji unakwenda kwa kasi na tatizo hilo litakabiliwa.

  Kutokana na uhaba uliopo, kwenye msimu wa mwaka 2016/17, baadhi ya wakulima walinunua magunia aina ya jute yanayotengenezwa Bangladesh na India.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako