• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • IGAD yaipongeza Marekani kwa kuondoa vikwazo vya kiuchumi dhidi ya Sudan

    (GMT+08:00) 2017-10-11 09:04:00

    Katibu mkuu wa Shirika la maendeleo la kiserikali ya nchi za Afrika Mashariki (IGAD) Balozi Mahboub Maalim, amepongeza kuondolewa kwa vikwazo vya biashara na uchumi ambavyo Marekani iliiwekea Sudan kwa miongo miwili iliyopita.

    Taarifa iliyotolewa na katibu mkuu huyo imesema, vikwazo hivyo vilivyowekwa na Marekani dhidi ya Sudan vimekuwa vizuizi vikubwa kwa utendaji wa kiuchumi, kisiasa, na kidiplomasia kwa nchi hiyo. Bw. Mahboub, kwa niaba yake na ya IGAD, ameipongeza serikali na watu wa Sudan kwa uvumilivu wao, matarajio mazuri, na uwezo wa kidiplomasia, licha ya changamoto ngumu walizokabiliwa nazo wakati wa miaka mingi ya kuwekewa vikwazo.

    Pia katibu mkuu huyo ameipongeza Marekani kwa uamuzi huo wa busara ambao utakuwa na athari nzuri, sio tu kwa uchumi wa Sudan, bali pia kwa nchi jirani pamoja na eneo lote la IGAD kwa ujumla. Bw. Maalim pia ametoa wito kwa serikali ya Marekani kufikiria kuiondoa Sudan kwenye orodha ya nchi zinazofadhili ugaidi.

    Wataalama wanasema, hatua hiyo ya Marekani ya kuiondolea Sudan vikwazo vya kiuchumi imeleta mabadiliko makubwa katika uhusiano wa nje wa Sudan, na kuashiria nchi hiyo kurudi kwenye mfumo wa fedha wa kimataifa. Wataalam hao wanasema kuwa kuondolewa kwa vikwazo hivyo kutaiwezesha Sudan kurejesha uhusiano wake wa kibiashara na kiuchumi na nchi nyingine, kurahisisha operesheni za kibenki na mchakato wa uagizaji na uingizaji. Pia hatua hiyo itarahisisha upatikanaji wa bidhaa, na pia huduma za afya na elimu, na pia kurejesha mawasiliano ya nchi hiyo na taasisi za kimataifa za fedha na uwekezaji.

    Kwa zaidi ya miaka 20, vikwazo vilivyowekwa na Marekani vilisababisha uharibifu mkubwa kwa uchumi wa Sudan, ikiwemo kuzuiliwa kwa zaidi ya dola milioni 7 za kimarekani zilizokuwa kwenye sekta ya benki nchini Sudan.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako