• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ofisa wa China aeleza changamoto zinazoikabili kazi ya kuondoa umaskini nchini China

    (GMT+08:00) 2017-10-11 09:23:42

    Mkurugenzi wa Ofisi ya upunguzaji umaskini kwenye Baraza la serikali la China Bw. Liu Yongfu amesema, kazi hiyo imepata mafanikio makubwa, lakini bado inakabiliwa na changamoto mbalimbali.

    Bw. Liu amesema bado kuna maeneo mengi yenye idadi kubwa ya watu maskini nchini China, na ni vigumu kukamilisha kazi ya kuondoa umaskini kwenye maeneo hayo katika miaka minne ijayo, haswa kwa wale walioangukia katika hali ya umaskini kutokana na magonjwa.

    Bw. Liu amesisitiza kuwa kazi kuu ya kipindi kijacho ni kufuata mwongozo wa kimkakati wa rais Xi Jinping kuhusu kupunguza umaskini, na kuendelea kutekeleza kwa kina malengo ya serikali kuu ya kuondoa umaskini, ili kufanikiwa katika mapambano dhidi ya umaskini.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako