• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Bara la Afrika linamatumaini kuandaa mashindano ya riadha 2025

  (GMT+08:00) 2017-10-11 09:26:27

  Rais wa shirikisho la riadha barani Afrika Hamad Malboum Kalkaba amesema kuwa ana imani kuwa bara la Afrika litaandaa mashindano ya riadha duniani mwaka 2025. Kwenye taarifa kwa wanahabari Kalkaba, amesema kuwa Kenya, Algeria, Misri, Morocco, Nigeria na Afrika Kusini zinauwezo wa kuandaa mbio hizo za dunia. Mashindano ya dunia ya mwaka 2019 yataandaliwa jijini Doha, Qatar ilihali yale ya mwaka 2021 yataandaliwa jijini Eugene, Oregon nchini Marekani. Jiji kuu la Hungary, Budapest limepigiwa upato wa kuandaa mbio hizo mwaka 2023. Kalkaba alithibitisha kuwa rais wa shirikisho la riadha duniani IAAF Sebastian Coe, ameunga mkono mipango hiyo. Malboum amesema kuwa ufanisi wa mashindano ya mbio za nyikani duniani jijini, Kampala, Uganda mwezi Machi na pia mashindano ya riadha kwa chipukizi duniani jijini Nairobi mwezi Julai ni udhihirisho kuwa Afrika iko tayari kuandaa mashindano hayo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako