• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Kuelekea kombe la dunia 2018 bara la Ulaya: Ureno, Ufaransa zakataka tiketi

  (GMT+08:00) 2017-10-11 09:26:54

  Andre Silva alifunga moja kati ya mabao mawili wakati Ureno wakiipiga Switzland bao 2 kwa nunge na kuifanya timu hiyo ya Ureno kukata rasmi tiketi ya kushiriki kombe la dunia mwakani nchini Urusi.

  Nayo timu ya taifa ya Ufaransa imewapiga Belarus goli 2-1 na kufuzu kwenda Urusi kushiriki michuano ya kombe la dunia huku ikiweka rekodi ya kutopoteza mchezo hata mmoja.

  Kule Ubelgiji nako watoto wawili katika familia moja ya mzee Hazard walishirikiana kuendeleza utemi wa Ubelgiji dhidi ya Cyprus kwa kuichabanga magoli 4-0.

  Timu ya taifa ya Uholanzi imekwama kufuzu kwa michuano hiyo licha ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Sweden, lakini haijatosha kuwapeleka kombe la dunia.

  Naye James McClean aipeleka Jamhuri ya Ireland, Urusi kwa kuifungia timu yake bao pekee dakika ya 57 ikiwalaza wenyeji Wales kwenye mchezo wa kundi D wa kufuzu kombe la dunia mwakani .

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako