• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Mpango wa ujenzi wa SGR Kisumu waamsha matumaini ya biashara ya kikanda

  (GMT+08:00) 2017-10-11 18:56:08

  Mpango wa ujenzi wa reli ya wastani maarufu kama standard gauge au SGR hadi mjini Kisumu umeongeza matumaini ya biashara ya kikanda wakati ambapo mji huo unaimarisha nafasi yake kama mojawapo ya vituo vya biashara Afrika Mashariki.

  Licha ya kuwa SGR inatarajiwa kujengwa hadi kwenye mpaka wa Malaba,wataalamu wanasema kuinganisha bandari ya Kisumu na ile ya Mombasa kunaonekana kama alama ya mwanzo kwa sababu kutaruhusu shehena kusafirishwa ziwa Victoria hadi nchi nyengine za Afrika Mashariki,na kuifanya SGR kuwa mradi wa kiuchumi unaofaa.

  Ujenzi wa SGR umeenda sanjari na ujenzi wa bandari katika ziwa victoria katika kijiji cha Usare,na kuongeza biashara kati ya Kenya na majirani zake kupitia Port Bell nchini Uganda,bandari ya Mwanza nchini Tanzania kupitia bandari ya Mwanza Sudan Kusini kupitia bandari ya Jinja na Rwanda kupitia Kimondo Bay.

  Kwa miongo mingi bandari ya Kisumu iliandikisha biashara kubwa ikisaidiwa na mfumo wa reli na vyombo vya majini ambavyo vilisafirisha shehena hadi bandari za Mwanza na Bukoba nchini Tanzania na Jinja na Port Bell nchini Uganda.

  Wenyeji wanasema bandari ya kisasa ya shehena huenda ikabadili mji wa Kisumu kuwa kituo cha biashara.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako