• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Uganda-URA imeenda mahakamani kuhusu ulipaji kodi katika uwanja wa ndege wa Entebbe

  (GMT+08:00) 2017-10-11 18:56:43

  Mamlaka ya mapato Uganda (URA) imewasilisha ombi katika mahakama ya haki ya Afrika Mashariki kupinga ada inayotozwa na Mamlaka ya Usafiri wa Anga (CAA).

  Inadaiwa kuwa tarehe 28 Agosti mwaka huu,CAA ilitoa mahitaji yasiyo ya kawaida ya kodi ya zaidi ya Shs5.3b na $52,557.98 dhidi ya URA kulingana na utumiaji wa sehemu katika uwanja wa ndege wa Entebbe.

  URA inatumia eneo la kuwasili na kituo cha mizigo kama kituo cha forodha ili kufanya shughuli zake za usimamizi na udhibiti wa forodha ikiwa ni pamoja na ukusanyaji mapato ya forodha.

  Inadaiwa kuwa CAA imetishia kuiondoa URA kutoka uwanja wa ndege kutokana na kukiukwa kwa usimamizi wa forodha katika uwanja huo wa ndege.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako