• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Tanzania:Maonyesho ya biashara yafungua fursa Burundi.

  (GMT+08:00) 2017-10-11 18:57:11

  Maonyesho ya biashara baina ya Burundi na Tanzania yaliyofanyika hivi karibuni jijini Daresalam yamefungua fursa ya biashara nchini Burundi kwa mujibu wa wizara ujenzi ya Burundi.

  Waziri wa Usafi rishaji na Ujenzi, wa Burundi Jean Bosco Ntunzwenimana amesema fursa mpya za ushirikiano kibiashara zimefunguka hususan katika sekta ya biashara ya bidhaa.

  Waziri huyo amesema Burundi itanufaika na itaendelea kufanya ushirikiano na Tanzania katika kupanua biashara na uwekezaji.

  Awali wafanyibiashara wa Burundi waliwekewa vikwazo kutumia Bandari maarufu ya Dar es Salaam lakiini sasa wanaitumia kupitishia mizigo yao kwa uhuru zaidi baada ya makubaliano ya serikali hizo .

  Serikali ya Tanzania imewapa nafuu ya kuwaondolea asilimia 40 ya gharama za kusafirisha mizigo kwa njia ya barabara.

  Aidha, Ntunzwenimana alisema kwa pamoja, Burundi na Tanzania zinaelekeza nguvu katika miradi mikubwa ya ujenzi.

  Miradi hiyo imelenga kukuza biashara na ustawi wa maendeleo baina ya nchi hizo, hivyo ni jambo la kujivunia.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako