• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • IMF yasema Zambia iko kwenye hatari kubwa ya kushindwa kulipa madeni

    (GMT+08:00) 2017-10-11 19:17:49

    Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) limeeleza wasiwasi wake kuhusu kasi ya deni la Zambia, hususan deni la nje ambalo limeongezeka na kuiweka nchi hiyo katika hatari kubwa ya kushindwa kulipa madeni hayo.

    Shirika hilo limesema Zambia inatakiwa kupunguza kasi ya kuongezeka kwa deni jipya, hususan mikopo isiyo na ridhaa, ili kudumisha utulivu wa madeni. Pia Shirika hilo limesema deni la umma la Zimbabwe limekuwa likiongezeka kwa kasi na kuielemea sekta binafsi, na hivyo kuongeza hatari kwa uchumi wa nchi hiyo.

    Takwimu za serikali ya Zambia zinaonyesha kuwa, deni la nchi hiyo limefikia dola za kimarekani bilioni 12.45 mpaka kufikia Agosti mwaka huu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako