• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Umoja wa Afrika wachangia msaada wa chakula kwa Somalia

    (GMT+08:00) 2017-10-11 19:18:06

    Kikosi cha Kulinda Amani cha Umoja wa Mataifa nchini Somalia AMISOM kimetoa msaada wa chakula wenye thamani ya dola za kimarekani laki moja kwa serikali ya Somalia ili kusaidia watu walioathirika na ukame.

    Taarifa iliyotolewa na Kikosi hicho imesema, chakula hicho ni pamoja na zaidi ya tani 67 za mchele, sukari, maharage, na mafuta ya kupikia. Mwakilishi maalum wa Kamati ya Umoja wa Afrika nchini Somalia Fransisco Madeira amesema hali nchini Somalia bado ni tete kutokana na uhaba wa mvua na mlipuko wa mara kwa mara wa magonjwa. Madeira amerejea tena ahadi ya AMISOM ya kuendelea kuunga mkono serikali ya Somalia na mashirika ya kibinadamu kuwafikia na kuwasaidia watu wanaohitaji msaada.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako