• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Bondia Larry Holmes amfagilia bondia Anthony Joshua

  (GMT+08:00) 2017-10-12 09:04:53

  Bingwa wa zamani wa dunia uzito wa juu katika mchezo wa masumbwi, Larry Holmes amesema kuwa kijana, Anthony Joshua atakuwa miongonini mwa mabondia bora kabisa wa muda wote siku za usoni.

  Holmes, ambaye ameshawahi kupigana na vigogo kama Mike Tyson na Muhammad Ali amesema bingwa huyo wa dunia wa WBA na IBF, Joshua atafikia hatua hiyo endapo ataendelea kuwa na jitihada katika mchezo wa ngumi. Bingwa huyo wa zamani mwenye umri wa miaka 67, amekiri kuvutiwa na kiwango kinachooneshwa na Joshua ambaye anatarajia kutetea mkanda wake Octoba 28 pale atakapo kabiliana na bondia, Kubrat Pulev kutoka Bulgaria katika uwanja wa Cardiff.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako