• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Rais wa Misri atoa zawadi ya dola 85,000 kwa timu ya taifa ya Misri baada ya kufuzu kombe la dunia

  (GMT+08:00) 2017-10-12 09:07:06

  Wikiendi iliyomalizika timu ya taifa ya Misri ilifanikiwa kufuzu kwenda kushiriki fainali za michuano ya Kombe la dunia nchini Urusi, kwa mara ya kwanza baada ya miaka 27, Misri wamefuzu kucheza fainali za kombe la dunia mwakani baada ya ushindi wa dakika za majeruhi wa magoli 2-1. Ushindi huo umewafanya Misri wafuzu moja kwa moja kutokana na kufikisha jumla ya point 12 ambazo haziwezi kufikiwa na timu yoyote ile ya Kundi E lililokuwa na timu za Uganda, Ghana na Congo Brazzaville licha ya kila timu kusalia na mchezo mmoja. Mara ya mwisho Misri kushiriki Kombe la Dunia ilikuwa mwaka 1990, miaka kabla ya Mohamed Salah kuzaliwa na zimepita fainali sita, hivyo kutokana na kiu ya muda mrefu Rais wa Misri Abdul Fattah al-Sisi ametoa zawadi ya dola 85,000 kwa kila mchezaji ambazo ni zaidi ya Tsh milioni 200 hiyo ni baada ya kukutana na kocha wao raia wa Argentina Hector Cuper.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako