• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Aubameyang asema ameamua mwenyewe kubaki Borussia Dortmund

  (GMT+08:00) 2017-10-12 09:07:29

  Mshambulaji wa Borussia Dortmund Pierre-Emerick Aubameyang amesema klabu yake ipo tayari kumuuza muda wowote lakini yeye ndio anaamua kubaki. Raia huyo wa Gabon amesema kuwa timu yake haijawahi kukataa kumuuza katika vipindi tofauti vya usajili vilivyopita lakini yeye ndio amekuwa akiweka ngumu kuondoka kwasababu anajisikia yupo nyumbani akiwa na timu hiyo.

  Mkali huyo wa mabao ameongeza kuwa kwasasa hafikirii kwenda popote pamoja na uwepo wa ofa kutoka vilabu tofauti tofuati lakini anajiona ana jukumu la kuitumikia zaidi Dortmund. Msimu uliopita Aubameyang mwenye miaka 28 alitwaa kiatu cha mfungaji bora katika ligi kuu ya soka ya Bundesliga na tayari msimu huu chini ya kocha mpya Peter Bosz ameshafunga mabao 13 katika michuano yote.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako