• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • UN yasema uhamishaji haramu wa fedha kutoka Afrika ni kikwazo katika kutimiza malengo ya maendeleo endelevu

    (GMT+08:00) 2017-10-12 09:26:13

    Mshauri maalum wa Umoja wa mataifa kuhusu malengo maendeleo endelevu kwenye kamati ya uchumi wa Afrika ya Umoja wa mataifa Bibi Aida Opoku Mensah, amesema dola bilioni 50 za kodi zinapotea kila mwaka kwa kupelekwa nje ya Afrika.

    Akiongea mjini Nairobi kwenye mkutano wa tano kuhusu usafirishaji fedha haramu na kodi kwa mwaka huu, Bibi Mensah amesema kuendelea kupotea kwa raslimali kunakwamisha juhudi za nchi za Afrika katika kutimiza malengo ya maendeleo endelevu.

    Kamati ya uchumi wa Afrika ya Umoja wa mataifa UNECA imesema uhamishaji haramu wa fedha barani Afrika unafanywa na mashirika ya kimataifa yanayofanya shughuli zake barani Afrika.

    Bibi Mensah ametaja kuwa usafirishaji huo haramu unafanywa kwa kupanga bei, makadirio ya chini ya bei, na kukwepa kodi, ili kupunguza kodi za makampuni hayo kwa serikali za nchi za Afrika.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako