• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Mahakama ya Iraq yatoa hati ya kukamatwa kwa waandaaji wa kura za maoni za jimbo la wakurd

  (GMT+08:00) 2017-10-12 09:34:36

  Mahakama ya Iraq imetoa hati ya kukamatwa kwa waandaaji wa kura za maoni latika jimbo la wakurd nchini Iraq. Msemaji wa mahakama hiyo Bw Abdul Sattar, ametoa taarifa akisema mahakama ya Baghdad imetoa hati ya kukamatwa kwa mwenyekiti na makamishina wa tume ya uchaguzi ya kura za maoni kwenye jimbo hilo.

  Hati hiyo ya kukamatwa imetolewa kutokana na maelekezo ya kamati ya usalama wa taifa inayoongozwa na waziri mkuu wa Iraq Bw Haider al-Abadi.

  Serikali ya Iraq imekuwa inapinga kura za maoni katika jimbo la wakurd kwa siku zote, na kuchukua hatua mbalimbali. Waziri mkuu wa Iraq Bw Haider al-Abadi amesisitiza tena kuwa serikali kuu ina msimamo imara, na italinda mshikamano na umoja wa nchi.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako