• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Waziri wa Rwanda alaani Shirika la Haki za Binadamu kuendelea kutoa shutuma zisizo na msingi

    (GMT+08:00) 2017-10-12 09:50:31

    Waziri wa sheria wa Rwanda Bw. Johnston Busingye amelilaani Shirika la kutetea haki za binadamu la Human Rights Watch, kwa kuendelea kutoa shutuma za zamani bila msingi wowote na bila ushahidi.

    Bw. Busingeye amesema hayo akijibu ripoti kuhusu kuwepo kwa vitendo vya jeshi kuwakamata watu mara kwa mara na kuwashikilia huku wakiwapiga, kuwakosesha hewa, kuwaua na kuwapiga shoti za umeme. Amesema Shirika la haki za binadamu linatumia shutuma hizo zisizo na msingi na kuendelea na ajenda yake ya kuipinga Rwanda.

    Jana Human Rights Watch lilitoa ripoti kuwa vitendo vya kukamata watu na kuwatesa vinaendelea kufanywa mara kwa mara na jeshi la Rwanda.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako