Ofisa mwandamizi wa Sudan Kusini amesema vyama mbalimbali vinavyounda serikali ya mpito ya umoja wa kitaifa, vimekubali kufanyika kwa majadiliano ya pamoja kuhusu kufufua makubaliano ya amani yaliyoandaliwa na Shirika la maendeleo la kiserikali ya nchi za Afrika Mashariki IGAD.
Waziri wa habari wa nchi hiyo Bw. Michael Makuei amesema, wamepokea barua kutoka kwa IGAD na kukubaliana kufanya majadiliano kwa pamoja, badala ya kufanya mazungumzo na chama kimoja kimoja.
Barua hiyo imekuja baada ya kiongozi wa chama cha SPLM-wapizani Bw. Dhieu Mathok kutoa wito kuhimiza kufanyika majadiliano ya pamoja.
Bw. Mathok amesisitiza kuwa serikali ya mpito ya umoja ya kitaifa ni chombo muhimu cha kutekeleza makubaliano ya amani.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |